Kauli ya Msanii
Usanikishaji wa Kitundu katika Ukumbi wa Tusher African Hall ni duka la mbele ambalo limepata hamasa yake kutoka kwa wale walio katika wilaya ya Kariakoo jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Kazi hiyo ni mkusanyiko wa marejeleo ya aina za maduka yanayopatikana katika eneo hilo na huelezwa kwa kumbukumbu za msanii na vyama.
Hili ni jibu kwa matumizi ya diorama kama zana za kufundishia na kwa historia yao yenye ugumu wa upatikanaji kama njia ya kuelimisha au kuburudisha hadhira ambayo iko mbali.
Diorama mara nyingi hutengenezwa kwa ustadi na mafundi wenye talanta za kustaajabisha. Zinastaajabisha kutazama lakini utengenezwaji wake uliokuwa sahihi ni kazi ya tamthiliya inayokusudiwa kusimulia hadithi.Karibu kila wakati hadithi hiyo inasimuliwa kwa mtazamo wa nje.
Kwa upande wa Bara la Afrika, diorama zilizojengwa Magharibi huwa zinaangalia kale, kuelekea mandhari ya asili "bora", na kupuuza mazingira yaliyojengwa kabisa.
Katika jamii isiyo na ufahamu kuhusu Afrika–ambayo mara chache hutafuta umaalum inapoongelea bara lenye watu bilioni moja na mara kwa mara hupokea taarifa zenye upotovu kuhusu nchi za Kiafrika na tamaduni zake – umbo la diorama kwa jinsi linavyotumika haitoi msingi wa watu katika uhalisia wa kuwepo kwetu.
Historia, maisha ya kisasa, na kazi ya kiakili na kisanii ya watu wa Kiafrika haipo, na kutokuwepo huku hakusumbui sana wale walio na fikra potovu za bara.
Kazi hii inakusudiwa kuwa uchochezi. Inakusudiwa kuonekana katika muktadha huu na kufikisha ujumbe wa kwamba watu kutoka Dar es Salaam–sio Waafrika tu kwa ujumla, na hasa zaidi wale wa wilaya ya Kariakoo–wanaishi, wanasikiliza, na wanaendelea na maisha yao ya kila siku ambayo ni ya kisasa.
Inakusudiwa kuwatoa wageni kutoka kwenye matembezi yaliyoboreshwa na ya kustaajabisha kupitia Ukumbi wa African Hall na kuwafanya washindane na uwepo wa bara kwa njia tofauti.
Hii ni fursa kwa maonyesho yote katika ukumbi kutazamwa kwa umakini zaidi na kuhakikisha kwamba mazungumzo kuhusu historia, ubinadamu, na mustakabali wetu wa pamoja yatafahamisha tafsiri zetu za ulimwengu asili.
Wasifu
Walter Kitundu ni Mtanzania-Mmarekani ambaye ni msanii wa fani mbalimbali na mwalimu Yeye huunda sanamu, hufanya usakinishaji wa sauti, na kazi za sanaa kubwa za umma zinazo ongelea mahali, historia, asili, na jamii.
Kitundu pia huunda ala za muziki zisizo za kawaida na vifaa vya kiufundi wakati ambapo anakili ulimwengu wa asili kama mpiga picha wa ndege. Kitundu ni mkurugenzi wa Kitundu Studio ambayo inajikita na ukuzaji na usanikishaji wa kazi za sanaa za umma. Alipokea Ushirika wa MacArthur Fellowship mnamo 2008 na pia ni Mshirika wa Osher Fellow.